Wanaume kama uliwahi kutendwa usifikiri wanawake wote wako hivyo




Kama kuna mwanamke aliwahi kukutenda huko nyuma, husifikirie kwamba wanawake wote wako hivyo. Maranyingi sana utaona kwasababu mwanamme huyo alipitia experience mbaya ya mahusiano,kwa msichana aliyetangulia basi utakuta analipiza mabaya kwa msichana mwingine.

Kuna mwanamke ambaye ni sahihi kwa ajili yako ambaye anatamani sana kukuthamini wewe kama anavyothaminiwa mfalme, ambaye yuko tayari kulitoa penzi lake kwako, ambaye anathamini mchango wako, jitihada zako, ambaye yuko tayari kukuheshimu wewe, ambaye ni mwoga kukuumiza na hata kukupoteza wewe.

Ambaye yuko tayari kuishi na wewe katika shida na raha siku zote za maisha yake na kujenga familia pamoja na wewe, ambaye atakupenda jinsi ulivyo na kukujali wewe kama mpenzi wake.Huyo msichana mvumilivu yupo kwaajili yako ni kiasi cha wewe kujua kwamba tatizo ni mda tu na inahitaji wewe kuwa mvumulivu.

Na pia inapotokea umempata basi husilipize mabaya kwa experience mbaya iliyopita, mpe nafasi ili uweze kumtambua na kumjua vizuri uliyenaye.

Nina uhakika umeishawahi kukutana na mtu wa aina hiyo katika maisha ya mahusiano yako.

Kuwa huru tuzungumze