MUIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, amedaiwa kumsaliti mpenzi wake wa siku nyingi, Chuchu Hans baada ya kukutwa akiwa amepozi kimahaba na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011, Husna Maulid katika Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar, hivi karibuni.
Wawili hao waliokuwa wamepakatana, walikutwa katika ukumbi huo wakati bendi mbili kubwa za muziki wa dansi nchini, FM Academia na The African Stars ‘Twanga Pepeta’ zilipokuwa zikiangusha burudani kabambe ya kushindana.
Uwepo wa Ray na Husna ulitafsiriwa kuwa ni usaliti kwani muda wote waliokuwa ndani ya ukumbi huo wawili hao walikuwa wamegandana kimahaba huku wataalamu wa ubuyu wakikazia madai kwa kusema wawili hao ni wapenzi.
“Sasa wewe kusoma hujui hata picha huoni? Hawa watakuwa ni wapenzi tu, haiwezekani mtu mpakatane, mpeane kampani kiasi hiki na mtu ambaye siyo mtu wako,” alisikika shuhuda mmoja.
Ray ambaye kabla ya kuwa na Chuchu aliwahi kutoka kimapenzi na mwigizaji Blandina Changula ‘Johari’ na Ruth Suka ‘Mainda’, alionekana kufurahia kumpakata Husna huku wakipeana kampani ya kuzungumza, lakini alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa akifuatiliwa na kamera ya paparazi wetu.
“Khaa! Unasemaje? Mimi siamini labda kama kuna picha zao za pamoja naomba unitumie Whatsapp nizione maana nashindwa niongee nini, sikujua kama walienda popote Ray na Husna.”
Mwanahabari wetu alimtumia picha hizo Chuchu lakini hadi tunakwenda mitamboni, mrembo huyo hakuwa amejibu kitu chochote.