Jamani, Usipoyajua Mapenzi Utayona Kama Usumbufu Vile.






Sikila mwanaume anajua maana ya kupendwa, wengine huona kufanya baadhi ya vitu ni usumbufu. Kwa mfano kuoshwa, kulishwa, kufanyiwa usafi wa sehemu za siri, kuvuliwa nguo au kubebwa mgongoni wanaume wengi huona usumbufu na hii hutegemea na makabila.
Jamanii, makubwa madogo yana nafuu, wakati watu wanalilia mapenzi kwa wenza wao kuna ambao wanaona eti ni usumbufu. Hii ilitokea juzi baada ya mtu na mkewe kuletana kwangu niliyoyasikia nilibakia kinywa wazi. Lakini baada ya kulifanyia kazi nilipata jibu kuwa huwezi kujibu mtihani bila kusoma unachotakiwa kujibu.
Mtoto wa Kitanga kaolewa na mwanaume toka Bara, mtoto ili kuongeza upendo kwa mume aliyafanya yote aliyopitia kwenye unyago ili mwanaume ajue kampata mwanamke mwenye silika ya kike, siyo mwanamke maumbile lakini tabia hata za kiume hana.
Unanishangaa nini? Ukweli ni huo uchukie ulie simo shida yangu uinywe japo chungu lakini ndiyo tiba yako. He! Nimeingia kwenye mada isiyonihusu hebu tuendelee na yetu. Basi mwari kila alilokuwa akilifanya kwa mumewe ilikuwa kama usumbufu. Akiambiwa panda mgongoni mwanaume wa watu anaona aibu na kulazimisha kwenda kuoga mwenyewe, kukata kucha hataki na kuogeshwa hataki.
Unajua utaona utani kuna wanaume wengine hata kuoga na wake zao huona aibu, uongo? Unamwangalia nini mkeo? Nazungumza na wewe, jamani mahaba yana nguzo zake kuna mambo yanataka uyajue mapema ukifanyiwa usishangae. Mmh! Nimekumbuka kuna siku katika pitapita yangu enzi zile niliangukia mikononi kwa mwanaume mmoja toka Bara, jamani mbona aibu kila nilichomfanyia kwake ilikuwa karaha yeye alichojua katika mapenzi ni kumdandia mwanamke na akimaliza shida zake kuondoka hata maandalizi hajui.
Jamani mi siwacheki kwa vile ndivyo walivyolelewa wengi mapenzi wameyaanzia ukubwani. Usifikiri ‘mashikolo mageni’ ni kwenye chakula tu hata kwenye mapenzi. Ukitumia mdomo anaruka anaona kama unataka kumtafuna. Usicheke inatia huruma watu hawa wanatakiwa kufundwa taratibu na mwisho wake watazoea na kujua kumbe mapenzi mpaka tendo la mwisho la kukutana kimwili yanapitia njia nyingi.
Basi baada ya kuyakumbuka yangu yaliyofanana na mwari wangu ambaye alikosa uhuru wa kuonesha aliyofundwa jinsi ya kumfanya wanaume apagawe, niliwaweka chini na kutoa mafunzo ambayo na wewe tega sikio hasa wewe wa Bara uliyezoea kupanda juu ya mnazi na kuangusha nazi kisha unateremka.
Jamani vitu hivi kwetu Pwani ni jambo la kawaida ambalo nina imani linaweza kuwa limesambaa nchi nzima. Wanawake tuliofundwa tumefundishwa kumlea mwanaume kama mtoto mdogo, usishangae kubebwa mgongoni, kupelekwa bafuni kisha kuoshwa kama mtoto huku mali zikiwa kwenye kisahani si unajua mwanaume bila mtaji huo utabakia mwanaume jina.
Baada ya kuoshwa kwa kusuguliwa kila kona utafutwa maji na kubebwa hadi ndani na kukalishwa kitandani kusubiri kupakwa mafuta na kulishwa chakula hapohapo kama mtoto. Baada ya chakula utamwachia uhuru mwenzako atafanya ziara mwilini kwa kutumia mikono laini na ulimi kuuchangamsha mwili kabla ya kuhitimisha zoezi la kurushana roho.
Vitu vyote hivi mwanaume anaweza kuvifanya mwenyewe kasoro kujibeba, lakini sisi tuliopitia unyagoni tunajua mwanaume afanyiwe nini ili kumtia mahanjamu, tukiwa tumevalia nguo za mitego ambazo zitamsisimua. 
Basi jamani, mapenzi usipoyajua utaona usumbufu, na ukiyajua utawahi kila siku nyumbani ufanyiwe. Watu wameuza nyumba za urithi baada ya kuangukia kwa wanaoyajua mapenzi. Raha ya kitu maandalizi mpe uhuru mpenzi wako akupe raha. Yangu leo yanatosha.