"Habari za kazi Mimi ni Mama wa miaka30 nimeolewa miaka miwili iliyopita na tumejaaliwa Mtoto mmoja. Mume wangu ni mtumishi mkubwa Serikalini.
Tatizo nililonalo dada na wadau wote ni kwamba Mume wangu nimetoka nae toka shule, kwenye mapenzi yetu hakuwahi kuninunulia hata chips!
Sikujali kabisa kwani nilielewa ni Dent baada ya muda nilishika mimba na nilipomueleza hakujibu kitu na akanitoroka kitu kilichopelekea kukosa kote Shule na Boyfrend.
Baadaye, zaidi ya miaka mitatu akantafuta na kuniomba msamaha kuwa ni kwasababu ya mazingira alokuwanayo akaogopa nakunikimbia. Nilimsamehe kwavile nilimpenda toka moyoni.
Kwajuhudi zangu binafsi nilikazana sana na shule hadi aliponitafuta nilikuwa Form6 na yeye akiwa chuo mwaka wa tatu lakini nilikuja kuhisi ubinafsi wake hapo kwani sikuwahi kupewa japo Kadi ingawa Chuo huwa tunapewa boom.
Nilifanikiwa kupata nafasi UDSMd nikamaliza vizuri. Mpenzi wangu huyo aliniomba kwa machozi anioe, nilimzungusha kwa miaka kadhaa then nikakubali.
Toka tumeoana ni vituko ndani ya nyumba, mara anisimange, mara nimfumanie na wanawake wakifanya starehe na kunikataa kuwa mie sio mkewe. Mara anifukuze kwa kudai namng'ang'ania anasema alikosea kunioa ili mradi tu ni manyanyaso.
Hanihudumii kwa chochote kile yaani sigusi gari lake, biashara zake wala hela zake. Hakai na document yoyote ndani anampa mama yake nazingine anaficha ofisini.
Amejenga nyumba kadhaa kwa siri, amenunua viwanja vingi tu hapa dar kwa siri, account zake ni za siri, miradi yake ananificha nakuja kuambiwa na mahawara zake wakijisifia kwangu.
Kwa kweli inaniumiza kupita kiasi hasa ukizingatia napenda kumtumikia MUNGU wangu lakini yeye hana hofu ya MUNGU. Anawaza ubinafsi, chuki, uchoyo na anataka nimpe mshahara wangu utumike nyumbani wakati yeye hajui wala kuhusika na mahitaji yangu.
Chaajabu nakuta anawatumia pesa wanawake wengine, mwingine anamwomba ampe gari, anawanunulia gold wakati mimi niliyemvumilia hata mia yake siioni!!
Hivi juzi kanunua Simu ya Milioni 1.5 wakati mie kisimu nachotumia Mungu anajua. Nimemuomba nikasome kanifokea kama mtoto!
Ndugu zangu anawachukia kuliko kawaida ila wake ndio anataka waje tukae nao. Jamani wapendwa nisaidieni, kama vikao tumeshakaa x3 anaomba msamaha na kuahidi kutorudia lakini wazazi na Wachungaji wakiondoka nakiona cha moto.
Ndoa nilofunga ni ya kikristo nami ni mdada mzuri sio najisifia bure hapana, msomi na mcha MUNGU siwezi kumsaliti ingawa natongozwa sana.
Mtoto wangu ndio kwanza ana mwaka lakini nimechoka. Nisaidieni ushauri jamani wapendwa".