SITOI RUSHWA YA NGONO KWA MAMENEJA..MSANII MAARUFU BONGO AFUNGUKA.


Staa wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda.

STAA wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda amewachana wasanii ‘wanaotembea’ na mameneja wao kwani ni ujinga wa mawazo na yeye kamwe hawezi kufanya hivyo.
Akizungumza na gazeti hili, Isabela alisema katika maisha yake hajawahi kuwa na uhusiano na meneja au prodyuza na huwa anawashangaa na kuwasikitikia wasanii wanaofanya hivyo wakati siyo njia sahihi ya kujikwamua kimuziki.