John alikuwa na hisia za mapenzi kwa binti mmoja siku nyingi sana. Lakini hakuweza kujieleza. Siku moja akajikakamua kumuandikia binti message "I love U so much!, Tafadhali nijibu hisia zako". Baada ya muda mchache simu yake iliingia msg nguvu zilimuisha kwa kutaka kujua binti kajibu nini... akaamua kulala asome msg siku inayofatia labda angepata ujasiri wa kuifungua msg. Siku iliyofuata jamaa akaamka mapema akafagia uwanja, akafanya usafi nyumba nzima na kazi zote mpaka watu wakamshangaa, mwishowe akaoga na kupata muda wa kupumzika na kujitupa kitandani kwa shauku ili aisome msg aliyojibiwa, kufungua msg akakuta................................ "Hauna salio la kutosha kutumia huduma hii, bonyeza *149*22# kupata Tigo niwezeshe. TIGO EXPRESS YOURSELF".