Nimegundua Mpenzi alizaa kabla, sina amani Ushauri



 Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 21 sijaolewa ila nina mchumba ambae ana malengo mazuri na mimi lakini dada nina tatizo moja.

Mchumba wangu huyu tangu niwe na uhusiano nae ni mwaka umepita sasa, kwa kweli ananipenda na mimi nampenda tena sana tu na ananihudumia kwa kila nitakacho yani kama mke wake. Huwa hanifichi kitu! lakini nimekuja kugudua kuwa yeye ana mtoto mmoja wa kike na ni mkubwa, kwanza alikataa kuniambia kwa kudai ni mapema mno baada ya kumbana akaniambia kweli kuwa anamtoto ambaye alizaa na mwanamke mmoja kabla ya kuwa na uhusiano na mimi.

Alidai kuwa anamuhudumia yule mwanamke sababu wazazi wa yule binti wamembana ahudumie, pia amesema yeye anampenda mtoto tu na sio mama yake kwani hakutaka kuzaa nae ila ilikuwa bahati mbaya!

Sasa dada mimi Moyo wangu umeingia chuki sana baada ya kusikia hivyo lakini mwenyewe anadai anampenda sana mtoto wake kuliko kitu kingine, mimi hapo ndio sielewi je anampenda kuliko mimi?

Dada naomba ushauri, huyu mwanaume nampenda na ndiye anayenisomesha Chuo mpaka sasa na huduma zote ananipa ila tatizo ni chuki iliyoniingia ghafla nashindwa kuelewa ni kwa nini naomba msaada wako! kwani nataka nafsi iwe na amani."